Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 95 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿قُل لَّوۡ كَانَ فِي ٱلۡأَرۡضِ مَلَٰٓئِكَةٞ يَمۡشُونَ مُطۡمَئِنِّينَ لَنَزَّلۡنَا عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَلَكٗا رَّسُولٗا ﴾
[الإسرَاء: 95]
﴿قل لو كان في الأرض ملائكة يمشون مطمئنين لنـزلنا عليهم من السماء﴾ [الإسرَاء: 95]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Waambie, ewe Muhammad, ukiwarudi washirikina kule kukanusha kwao kuwa Mtume ni miongoni mwa wanadamu, «Lau juu ya hii ardhi kulikuwa na Malaika wanatembea kwa kujituliza, tungaliwapelekea mtume miongoni mwa jinsi yao,» lakini watu wa ardhi ni wanadamu, basi mtume wa kupelekewa inatakiwa awe ni miongoni mwa jinsi yao, ili iwezekane kwao kuzungumza naye na kufahamu maneno yake |