Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 99 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿۞ أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّ ٱللَّهَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يَخۡلُقَ مِثۡلَهُمۡ وَجَعَلَ لَهُمۡ أَجَلٗا لَّا رَيۡبَ فِيهِ فَأَبَى ٱلظَّٰلِمُونَ إِلَّا كُفُورٗا ﴾
[الإسرَاء: 99]
﴿أو لم يروا أن الله الذي خلق السموات والأرض قادر على أن﴾ [الإسرَاء: 99]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, kwani wameghafilika hawa washirikina, wasiangalie na kujuwa kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyeumba mbingu na ardhi na viumbe vilivyomo ndani yake bila ya mfano uliotangulia, ni muweza wa kuumba mfano wao baada ya kumalizika kwao? Mwenyezi Mungu Amewaekea washirikina hawa wakati maalumu wa kufa kwao na kuadhibiwa, hapana shaka wakati huo utawafikia. Na pamoja na uwazi wa haki na dalili Zake walikataa washirikina isipokuwa ni kuikanusha Dini ya Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka |