Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 100 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿قُل لَّوۡ أَنتُمۡ تَمۡلِكُونَ خَزَآئِنَ رَحۡمَةِ رَبِّيٓ إِذٗا لَّأَمۡسَكۡتُمۡ خَشۡيَةَ ٱلۡإِنفَاقِۚ وَكَانَ ٱلۡإِنسَٰنُ قَتُورٗا ﴾
[الإسرَاء: 100]
﴿قل لو أنتم تملكون خزائن رحمة ربي إذا لأمسكتم خشية الإنفاق وكان﴾ [الإسرَاء: 100]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Lau nyinyi mnamiliki hazina za rehema ya Mola wangu ambazo hazimaliziki wala hazitoeki, basi mungalizifanyia ubahili msitoe katika hizo kuwapa wengine kwa kuchelea zisimalizike mkawa mafukara.» Na ni katika tabia ya binadamu kuwa yeye ni mgumu wa kile kilicho mkononi mwake, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu |