Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 31 - الكَهف - Page - Juz 15
﴿أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ جَنَّٰتُ عَدۡنٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمُ ٱلۡأَنۡهَٰرُ يُحَلَّوۡنَ فِيهَا مِنۡ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٖ وَيَلۡبَسُونَ ثِيَابًا خُضۡرٗا مِّن سُندُسٖ وَإِسۡتَبۡرَقٖ مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِۚ نِعۡمَ ٱلثَّوَابُ وَحَسُنَتۡ مُرۡتَفَقٗا ﴾
[الكَهف: 31]
﴿أولئك لهم جنات عدن تجري من تحتهم الأنهار يحلون فيها من أساور﴾ [الكَهف: 31]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hao walioamini watakuwa na mabustani ya Peponi, watakaa humo daima, ambapo mito yenye maji tamu itakuwa ikipita chini ya vyumba vyao na nyumba zao. Watapambwa humo kwa vikuku vya dhahabu, na watavaa nguo za rangi ya kijani zilizofumwa kwa hariri nyembamba na nzito. Watategemea wakiwa humo kwenye vitanda vilivopambwa kwa pazia nzuri. Neema ya malipo ni malipo yao, na Pepo ni nzuri kuwa ni mashukio yao na mahali pao |