Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 42 - الكَهف - Page - Juz 15
﴿وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِۦ فَأَصۡبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيۡهِ عَلَىٰ مَآ أَنفَقَ فِيهَا وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُشۡرِكۡ بِرَبِّيٓ أَحَدٗا ﴾
[الكَهف: 42]
﴿وأحيط بثمره فأصبح يقلب كفيه على ما أنفق فيها وهي خاوية على﴾ [الكَهف: 42]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yakawa ni kweli yale maneno ya yule Muumini, na shamba likaharibika na vilivyomo ndani vikaangamia, akawa yule kafiri anageuza vitanga vyake vya mikono huku na huku kwa kulilia hasara na majuto kwa gharama aliyoitoa pale, na hali mitiyake imeanguka chini baadhi yake iko juu ya mingine, na akawa yuwasema, «Natamani lau nilizitambua neema za Mwenyezi Mungu na uweza Wake na sikumshirikisha Mwenyezi Mungu na yoyote.» Na haya ni majuto yake wakati ambapo majuto hayamfalii kitu |