Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 82 - الكَهف - Page - Juz 16
﴿وَأَمَّا ٱلۡجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَٰمَيۡنِ يَتِيمَيۡنِ فِي ٱلۡمَدِينَةِ وَكَانَ تَحۡتَهُۥ كَنزٞ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَٰلِحٗا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبۡلُغَآ أَشُدَّهُمَا وَيَسۡتَخۡرِجَا كَنزَهُمَا رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۚ وَمَا فَعَلۡتُهُۥ عَنۡ أَمۡرِيۚ ذَٰلِكَ تَأۡوِيلُ مَا لَمۡ تَسۡطِع عَّلَيۡهِ صَبۡرٗا ﴾
[الكَهف: 82]
﴿وأما الجدار فكان لغلامين يتيمين في المدينة وكان تحته كنـز لهما وكان﴾ [الكَهف: 82]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Na ama ukuta nilioulinganisha, baada ya kuwa umeinama, mpaka ukawa sawa, ulikuwa ni wa wavulana wawili mayatima hapo kijijini, na chini yake kulikuwa na hazina yao ya dhahabu na fedha, na baba yao alikuwa mtu mwema, Mola wako Akataka wawe wakubwa, wapate nguvu na waitoe hazina yao kwa rehema itokayo kwa Mola wako. Na mimi sikuyafanya yote haya, ewe Mūsā, kwa amri yangu na kivyangu, kwa hakika nimeyafanya kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hayo niliyokueleza sababu zake ndiyo mwisho wa mambo ambayo hukuweza kuyavumilia kwa kuacha kuyauliza na kunipinga kwayo.» |