Quran with Swahili translation - Surah Maryam ayat 21 - مَريَم - Page - Juz 16
﴿قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٞۖ وَلِنَجۡعَلَهُۥٓ ءَايَةٗ لِّلنَّاسِ وَرَحۡمَةٗ مِّنَّاۚ وَكَانَ أَمۡرٗا مَّقۡضِيّٗا ﴾
[مَريَم: 21]
﴿قال كذلك قال ربك هو علي هين ولنجعله آية للناس ورحمة منا﴾ [مَريَم: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Malaika akasema kumwambia, «Mambo ni hivyo kama unavyoeleza kwamba hakuna binadamu aliyekugusa na hukuwa mzinifu, lakini Mola wako Amesema, ‘Jambo hili kwangu ni pesi, na ili mtoto huyu awe ni alama kwa watu yenye kuonesha uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na awe ni rehema itakayotokana na sisi kwake yeye, kwa mamake na kwa watu.’» Na kupatikana kwa Īṣā kinamna hii lilikuwa ni jambo lililokadiriwa katika Ubao uliohifadhiwa, basi hapana budi lifanyike |