Quran with Swahili translation - Surah Maryam ayat 37 - مَريَم - Page - Juz 16
﴿فَٱخۡتَلَفَ ٱلۡأَحۡزَابُ مِنۢ بَيۡنِهِمۡۖ فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن مَّشۡهَدِ يَوۡمٍ عَظِيمٍ ﴾
[مَريَم: 37]
﴿فاختلف الأحزاب من بينهم فويل للذين كفروا من مشهد يوم عظيم﴾ [مَريَم: 37]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mapote ya watu wa Kitabu walitafautiana baina yao kuhusu mambo ya Īsā, amani imshukiye, kati yao kuna wanaopita kiasi katika kumtukuza nao ni Wanaswara, kati yao kuna waliosema kuwa yeye ni Mwenyezi Mungu, kati yao kuna waliosema kuwa yeye ni mwana wa Mwenyezi Mungu, kati yao kuna waliosema kuwa yeye ni mmoja kati ya waungu watatu, Ametukuka Mwenyezi Mungu na kuwa mbali na hilo wanalolisema, na kati yao kuna waliomwepuka, nao ni Mayahudi, na wakasema kwamba yeye ni mchawi na wakasema kwamba yeye ni mwana wa Yūsuf aliyekuwa seremala. Basi maangamivu ni ya waliokanusha kuwa wataishuhudia siku yenye vituko vikubwa, nayo ni Siku ya Kiyama |