×

WAPUMBAVU miongoni mwa watu watasema: Nini kilicho wageuza kutoka kibla chao walicho 2:142 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:142) ayat 142 in Swahili

2:142 Surah Al-Baqarah ayat 142 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 142 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿۞ سَيَقُولُ ٱلسُّفَهَآءُ مِنَ ٱلنَّاسِ مَا وَلَّىٰهُمۡ عَن قِبۡلَتِهِمُ ٱلَّتِي كَانُواْ عَلَيۡهَاۚ قُل لِّلَّهِ ٱلۡمَشۡرِقُ وَٱلۡمَغۡرِبُۚ يَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ ﴾
[البَقَرَة: 142]

WAPUMBAVU miongoni mwa watu watasema: Nini kilicho wageuza kutoka kibla chao walicho kuwa wakikielekea? Sema: Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu; Yeye humwongoa amtakaye kwenye njia iliyo nyooka

❮ Previous Next ❯

ترجمة: سيقول السفهاء من الناس ما ولاهم عن قبلتهم التي كانوا عليها قل, باللغة السواحيلية

﴿سيقول السفهاء من الناس ما ولاهم عن قبلتهم التي كانوا عليها قل﴾ [البَقَرَة: 142]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Watasema wajinga na madhaifu wa akili, miongoni mwa Mayahudi na mfano wao, wakiwa katika hali ya kufanya maskhara na kupinga, «Ni kitu gani kilichowageuza hawa Waislamu kuacha kibla chao ambacho walikuwa wakisali kukielekea mwanzo wa Uislamu?»(Nacho ni Baitul Maqdis). Waambie, ewe Mtume, «Upande wa Mashariki na wa Magharibi na katikati yake ni milki ya Mwenyezi Mungu. Hapana upande wowote, miongoni mwa pande zote, ulioko nje ya milki Yake. Yeye Anamuongoza Amtakaye, miongoni mwa waja Wake, kumuelekeza njia ya uongofu iliyo sawa.» Katika hayo, pana ujulishaji kwamba mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu, katika kufuata amri Zake, na kwa hivyo, popote tuelekezwapo tutaelekea
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek