Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 148 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَلِكُلّٖ وِجۡهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَاۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ أَيۡنَ مَا تَكُونُواْ يَأۡتِ بِكُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ ﴾
[البَقَرَة: 148]
﴿ولكل وجهة هو موليها فاستبقوا الخيرات أين ما تكونوا يأت بكم الله﴾ [البَقَرَة: 148]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kila ummah, miongoni mwa ummah wa kila aina, una kibla chake anachokielekea kila mmoja katika wao kwenye swala yake. Basi kimbilieni, enyi Waumini, hali ya kushindana katika kutenda vitendo vyema ambavyo Ameviwajibisha kwenu Mwenyezi Mungu katika Dini ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu Atawakusanya nyote Siku ya Kiyama kutoka popote mtakapokuwa. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu |