×

Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo 2:150 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:150) ayat 150 in Swahili

2:150 Surah Al-Baqarah ayat 150 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 150 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَحَيۡثُ مَا كُنتُمۡ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ شَطۡرَهُۥ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيۡكُمۡ حُجَّةٌ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِي وَلِأُتِمَّ نِعۡمَتِي عَلَيۡكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ ﴾
[البَقَرَة: 150]

Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na ili mpate kuongoka

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ومن حيث خرجت فول وجهك شطر المسجد الحرام وحيث ما كنتم فولوا, باللغة السواحيلية

﴿ومن حيث خرجت فول وجهك شطر المسجد الحرام وحيث ما كنتم فولوا﴾ [البَقَرَة: 150]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na mahali popote utokapo, ewe Nabii, elekea Msikiti wa Haram. Na popote mnapokuwa, enyi Waislamu, katika nchi yoyote miongoni mwa nchi za ardhi, elekezeni nyuso zenu upande wa Msikiti wa Haram, ili watu wapinzani wasiwe na hoja yoyote kwenu kwa njia ya ugomvi na mjadala, baada ya kuelekea huko, isipokuwa wale madhalimu na wenye ukaidi kati yao. Hao watabakia kwenye mjadala wao. Basi, msiwaogope wao, niogopeni Mimi kwa kufuata amri Yangu na kujiepusha na katazo Langu na ili nikamilishe neema Zangu kwenu kuwachagulia sheria zilizokamilika zaidi, na ili mpate kuongoka kufuata haki na usawa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek