Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 183 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ ﴾
[البَقَرَة: 183]
﴿ياأيها الذين آمنوا كتب عليكم الصيام كما كتب على الذين من قبلكم﴾ [البَقَرَة: 183]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi ambao mumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mukaifuata Sheria Yake kivitendo, Mwenyezi Mungu Amewafaradhia kufunga, kama Alivyowafaradhia uma waliokuweko kabla yenu, ili mupate kumcha Mola wenu na kuweka kinga kati yenu na maasia, kwa kumtii na kumuabudu Peke Yake |