Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 182 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿فَمَنۡ خَافَ مِن مُّوصٖ جَنَفًا أَوۡ إِثۡمٗا فَأَصۡلَحَ بَيۡنَهُمۡ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 182]
﴿فمن خاف من موص جنفا أو إثما فأصلح بينهم فلا إثم عليه﴾ [البَقَرَة: 182]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi yoyote atakayejua kuwa mwenye kuusia amepinduka, kwa kuiacha haki katika wasia wake kwa njia ya kukosea au kukusudia, akamnasihi mtoaji wasia, wakati wa kutoa wasia, afanye uadilifu, na iwapo hilo halikuwa akaleta upatanishi kati ya pande zinazohusika kwa kugeuza wasia ili ulingane na Sheria, basi atakuwa hana dhambi katika kupatanisha huku. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kuwasamehe waja wake, ni Mwenye huruma kwao |