×

Watu wote walikuwa ni umma mmoja. Mwenyezi Mungu akapeleka Manabii wabashiri na 2:213 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:213) ayat 213 in Swahili

2:213 Surah Al-Baqarah ayat 213 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 213 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿كَانَ ٱلنَّاسُ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ فَبَعَثَ ٱللَّهُ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَ ٱلنَّاسِ فِيمَا ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِۚ وَمَا ٱخۡتَلَفَ فِيهِ إِلَّا ٱلَّذِينَ أُوتُوهُ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۖ فَهَدَى ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لِمَا ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِ مِنَ ٱلۡحَقِّ بِإِذۡنِهِۦۗ وَٱللَّهُ يَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٍ ﴾
[البَقَرَة: 213]

Watu wote walikuwa ni umma mmoja. Mwenyezi Mungu akapeleka Manabii wabashiri na waonyaji. Na pamoja nao akateremsha Kitabu kwa Haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale walio khitalifiana. Na wala hawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hicho baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu kwa idhini yake akawaongoa walio amini kwendea haki katika mambo waliyo khitalifiana. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka

❮ Previous Next ❯

ترجمة: كان الناس أمة واحدة فبعث الله النبيين مبشرين ومنذرين وأنـزل معهم الكتاب, باللغة السواحيلية

﴿كان الناس أمة واحدة فبعث الله النبيين مبشرين ومنذرين وأنـزل معهم الكتاب﴾ [البَقَرَة: 213]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Watu walikuwa ni kundi moja, wameafikiana katika kumuamini Mwenyezi Mungu, kisha walitafautiana katika dini yao.Hapo ndipo Mwenyezi Mungu Aliwatuma Manabii, wakiwa ni walinganizi wa dini ya Mwenyezi Mungu, ni wabashiri wa Pepo kwa anayemtii Mwenyezi Mungu na ni waonyi wa Moto kwa anayemkanusha na kumuasi. Na Akateremsha, pamoja nao, vitabu vya mbinguni vilivyokusanya haki, ili wahukumu baina ya watu kwa yaliyomo ndani, katika yale waliyotafautiana juu yake. Na hawakutafautiana juu ya jambo la Mtume na Kitbu alichokuja nacho, kwa uhasidi na udhalimu, isipokuwa ni wale ambao Mwenyezi Mungu Amewapa Taurati na wakayajua yaliyomo ndani miongoni mwa hoja na hukumu. Hapo Mwenyezi Mungu, kwa fadhila zake, aliwaafikia Waumini kuipambanua haki na batili na kuyajua yale waliotafautiana juu yake. Mwenyezi Mungu Anampa taufiki amtakaye, miongoni mwa waja wake, kufuata njia iliyonyooka
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek