Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 214 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿أَمۡ حَسِبۡتُمۡ أَن تَدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ وَلَمَّا يَأۡتِكُم مَّثَلُ ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلِكُمۖ مَّسَّتۡهُمُ ٱلۡبَأۡسَآءُ وَٱلضَّرَّآءُ وَزُلۡزِلُواْ حَتَّىٰ يَقُولَ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ مَتَىٰ نَصۡرُ ٱللَّهِۗ أَلَآ إِنَّ نَصۡرَ ٱللَّهِ قَرِيبٞ ﴾
[البَقَرَة: 214]
﴿أم حسبتم أن تدخلوا الجنة ولما يأتكم مثل الذين خلوا من قبلكم﴾ [البَقَرَة: 214]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani mlidhani, enyi Waumini, kwamba mtaingia Peponi, na bado haijawapata mitihani kama ile iliyowapata Waumini waliopita kabla yenu: ya ufukara, maradhi, kitisho na babaiko, na wakatikiswa kwa aina nyingi za misukosuko ya kutisha, mpaka akasema Mtume wao na Waumini pamoja naye, kwa njia ya kuharakisha nusura ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, «Ni lini hiyo nusura ya Mwenyezi Mungu?» Jueni kwamba nusura ya Mwenyezi Mungu iko karibu na Waumini |