×

Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa 2:219 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:219) ayat 219 in Swahili

2:219 Surah Al-Baqarah ayat 219 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 219 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿۞ يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡخَمۡرِ وَٱلۡمَيۡسِرِۖ قُلۡ فِيهِمَآ إِثۡمٞ كَبِيرٞ وَمَنَٰفِعُ لِلنَّاسِ وَإِثۡمُهُمَآ أَكۡبَرُ مِن نَّفۡعِهِمَاۗ وَيَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَۖ قُلِ ٱلۡعَفۡوَۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَتَفَكَّرُونَ ﴾
[البَقَرَة: 219]

Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri

❮ Previous Next ❯

ترجمة: يسألونك عن الخمر والميسر قل فيهما إثم كبير ومنافع للناس وإثمهما أكبر, باللغة السواحيلية

﴿يسألونك عن الخمر والميسر قل فيهما إثم كبير ومنافع للناس وإثمهما أكبر﴾ [البَقَرَة: 219]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wanakuuliza Waislamu, ewe Nabii, hukumu ya kutumia khamr kwa kunywa, kuuza na kununua. Khamr ni kila chenye kulewesha kinachofinika akili na kuziba, kiwe ni chenye kunywewa au kuliwa. Na wanakuuliza kuhusu hukumu ya kamari. Kamari ni kupokea au kutoa mali kwa bahati nasibu, nayo ni mashindano ambayo yana kupeana badali kutoka pande mbili za ushindani. Waambie, «Katika hayo pana madhara mengi na uharibifu mwingi katika dini na dunia, na akili na mali. Na yamo, katika mambo mawili hayo, manufaa kwa watu, kwa upande wa kuchuma mali na mengineyo. Na madhambi yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake, kwani huzuia kumtaja Mwenyezi Mungu na kusali, na yote mawili yanaleta uadui na kuchukiana kati ya watu na yanaharibu mali. Huu ulikuwa ni utayarishaji wa kuyaharamisha mambo mawili hayo. Na wanakuuliza kuhusu kiwango ambacho wao wakitoe katika mali yao kwa njia ya sadaka na kujitolea.Waambie, «Toeni kiwango kinachozidi baada ya mahitaji yenu.» Mfano wa haya maelezo yaliyo wazi, Mwenyezi Mungu Anawabainishia aya na hukumu za Sheria, ili mpate kuyafikiria yenye manufaa kwenu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek