Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 220 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۗ وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡيَتَٰمَىٰۖ قُلۡ إِصۡلَاحٞ لَّهُمۡ خَيۡرٞۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمۡ فَإِخۡوَٰنُكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ ٱلۡمُفۡسِدَ مِنَ ٱلۡمُصۡلِحِۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَأَعۡنَتَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 220]
﴿في الدنيا والآخرة ويسألونك عن اليتامى قل إصلاح لهم خير وإن تخالطوهم﴾ [البَقَرَة: 220]
Abdullah Muhammad Abu Bakr duniani na Akhera. Na wanakuuliza, ewe Mtume, kuhusu mayatima, waingiliane nao vipi katika maisha yao na mali yao. Waambie, «Kuwatengezea kwenu mambo yao ni bora. Basi, wafanyieni daima yanayowafaa wao zaidi.Na iwapo mtatangamana nao katika mambo ya maisha, basi wao ni ndugu zenu katika Dini. Na ni juu ya ndugu kuyalinda maslahi ya ndugu yake.Mwenyezi Mungu Anamjua mpotezaji wa mali ya mayatima na yule mwenye pupa la kuyahifadhi. Na lau Mwenyezi Mungu Angetaka, angewatia dhiki na mashaka kwa kuwaharamishia mtangamano. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwingi wa hekima katika uumbaji Wake, uendeshaji mambo Wake na upitishaji sheria Wake |