Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 247 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَقَالَ لَهُمۡ نَبِيُّهُمۡ إِنَّ ٱللَّهَ قَدۡ بَعَثَ لَكُمۡ طَالُوتَ مَلِكٗاۚ قَالُوٓاْ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ عَلَيۡنَا وَنَحۡنُ أَحَقُّ بِٱلۡمُلۡكِ مِنۡهُ وَلَمۡ يُؤۡتَ سَعَةٗ مِّنَ ٱلۡمَالِۚ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰهُ عَلَيۡكُمۡ وَزَادَهُۥ بَسۡطَةٗ فِي ٱلۡعِلۡمِ وَٱلۡجِسۡمِۖ وَٱللَّهُ يُؤۡتِي مُلۡكَهُۥ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 247]
﴿وقال لهم نبيهم إن الله قد بعث لكم طالوت ملكا قالوا أنى﴾ [البَقَرَة: 247]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mtume wao aliwaambia, «Hakika Mwenyezi Mungu Amewaltea Tālūt kuwa ni mfalme, ikiwa ni kuyaitikia maombi yenu, ili awaongoze katika kupigana na adui yenu kama mlivyoomba.» Wakasema wakuu wa Wana wa Isrāīl, «Vipi Tālūt atakuwa mfalme kwetu, hali yeye hastahiki hilo? Yeye si katika wajukuu wa wafalme, wala hatoki kwenye nyumba ya utume na wala hakupewa ukunjufu wa mali ya kujisaidia nayo katika ufalme wake. Sisi tuna haki zaidi ya huu ufalme kuliko yeye. Kwani sisi ni wajukuu wa wafalme na tunatoka kwenye nyumba ya utume.» Mtume wao akawaambia, «Hakika Mwenyezi Mungu Amewachagulia, na Yeye, Aliyetakasika na kila sifa mbaya, Anayajua zaidi mambo ya waja Wake, na Amemuengezea ukunjufu wa elimu na nguvu ya mwili ya kupigana na adui. Na Mwenyezi Mungu ni Mmiliki wa ufalme. Anampa ufalme wake Anayemtaka katika waja wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa fadhila na utoaji, ni Mjuzi kabisa wa ukweli wa mambo, hapana chenye kufichika Kwake.» |