Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 28 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿كَيۡفَ تَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَكُنتُمۡ أَمۡوَٰتٗا فَأَحۡيَٰكُمۡۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمۡ ثُمَّ يُحۡيِيكُمۡ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ﴾
[البَقَرَة: 28]
﴿كيف تكفرون بالله وكنتم أمواتا فأحياكم ثم يميتكم ثم يحييكم ثم إليه﴾ [البَقَرَة: 28]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Vipi mtaukanusha, enyi washirikina, umoja wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kumshirikisha mwengine katika Ibada, pamoja na kuwa kuna dalili zisizopingika kuhusu hilo katika nafsi zenu? Mlikuwa hamko, hamjaumbwa, Akawafanya muweko kwa kuwaumba, Akapuliza kwenu uhai, kisha Atawafisha baada ya kumalizika muda wenu wa kuishi Aliowaekea, kisha Atawarudisha mkiwa na uhai Siku ya Kufufuliwa, kisha mtarejeshwa Kwake mhesabiwe na mlipwe |