Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 49 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَإِذۡ نَجَّيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 49]
﴿وإذ نجيناكم من آل فرعون يسومونكم سوء العذاب يذبحون أبناءكم ويستحيون نساءكم﴾ [البَقَرَة: 49]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kumbukeni neema Yetu juu yenu, tulipowaokoa nyinyi na mateso ya Fir'awn na wafuasi wake, waliokuwa wakiwaonjesha nyinyi adhabu kali sana, wakiwaua watoto wenu wa kiume kwa wingi na kuwaacha wanawake wenu kwa kutumika na kudhalilishwa. Katika hilo, ni mtihani kwenu kutoka kwa Mola wenu. Na katika kuokolewa kwenu na yeye, ni neema kubwa ambayo inapasa kwenu mumshukuru Mwenyezi Mungu Aliyetukuka katika kila zama zenu na vizazi vyenu |