Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 50 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَإِذۡ فَرَقۡنَا بِكُمُ ٱلۡبَحۡرَ فَأَنجَيۡنَٰكُمۡ وَأَغۡرَقۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ ﴾
[البَقَرَة: 50]
﴿وإذ فرقنا بكم البحر فأنجيناكم وأغرقنا آل فرعون وأنتم تنظرون﴾ [البَقَرَة: 50]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kumbukeni neema Yetu juu yenu, tulipoipambanua bahari kwa ajili yenu na tukafanya ndani yake njia kavu, mkavuka na tukawaokoa na Fir'awn na askari wake na msizame majini. Fir'awn na askari wake walipoingia kwenye njia mlizopitia, tuliwazamisha majini mbele ya macho yenu |