Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 81 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿بَلَىٰۚ مَن كَسَبَ سَيِّئَةٗ وَأَحَٰطَتۡ بِهِۦ خَطِيٓـَٔتُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ﴾
[البَقَرَة: 81]
﴿بلى من كسب سيئة وأحاطت به خطيئته فأولئك أصحاب النار هم فيها﴾ [البَقَرَة: 81]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hukumu ya Mwenyezi Mungu imethibiti kwamba mwenye kutenda makosa mpaka yakamtia ukafirini na madhambi yake yakamtawala yeye sehemu zake zote, na hali hii haiwi isipokuwa kwa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, wote hao, washirikina na makafiri, ndio wenye kukaa Motoni makao ya milele yasiyokatika |