Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 91 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ ءَامِنُواْ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُواْ نُؤۡمِنُ بِمَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا وَيَكۡفُرُونَ بِمَا وَرَآءَهُۥ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَهُمۡۗ قُلۡ فَلِمَ تَقۡتُلُونَ أَنۢبِيَآءَ ٱللَّهِ مِن قَبۡلُ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ﴾
[البَقَرَة: 91]
﴿وإذا قيل لهم آمنوا بما أنـزل الله قالوا نؤمن بما أنـزل علينا﴾ [البَقَرَة: 91]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na baadhi ya Waislamu wanaposema kuwaambia Mayahudi, “Aminini Qur’ani,” wanasema, “Sisi tunaviamini vilivyoteremshwa kwa Mitume wetu.” Na wao wanakanusha vilivyoteremshwa na Mwenyezi Mungu baada yake, pamoja na kuwa ndio haki inayosadikisha vile walivyonavyo. Lau wao walikuwa wanaviamini vitabu vyao kikweli, wangaliiamini Qur’ani iliyozisadikisha. Waambie, ewe Mtume, “Iwapo nyinyi mnayamini yale mliyoteremshiwa na Mwenyezi Mungu kwenu, kwa nini mliwaua Manabii wa Mwenyezi Mungu wakati wa nyuma?” |