×

Kiovu kweli walicho jiuzia nafsi zao, nacho ni kule kukataa kwao aliyo 2:90 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:90) ayat 90 in Swahili

2:90 Surah Al-Baqarah ayat 90 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 90 - البَقَرَة - Page - Juz 1

﴿بِئۡسَمَا ٱشۡتَرَوۡاْ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمۡ أَن يَكۡفُرُواْ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بَغۡيًا أَن يُنَزِّلَ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ فَبَآءُو بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٖۚ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٞ مُّهِينٞ ﴾
[البَقَرَة: 90]

Kiovu kweli walicho jiuzia nafsi zao, nacho ni kule kukataa kwao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kuona maya kwa kuwa Mwenyezi Mungu humteremshia fadhila yake amtakaye miongoni mwa waja wake. Basi wamejiletea wenyewe ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata mateso ya kudhalilisha

❮ Previous Next ❯

ترجمة: بئسما اشتروا به أنفسهم أن يكفروا بما أنـزل الله بغيا أن ينـزل, باللغة السواحيلية

﴿بئسما اشتروا به أنفسهم أن يكفروا بما أنـزل الله بغيا أن ينـزل﴾ [البَقَرَة: 90]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Ni baya chaguo la Wana wa Isrāīl walilojichagulia. Kwani walibadilisha imani kwa ukafiri, (kwa kuacha imani na kuchukua ukafiri) kwa dhulma na uhasidi kwa kuwa Mwenyezi Mungu, kwa fadhila ZAke, Alimteremshia Nabii Wake na Mtume Wake Muhammad, rehema na amani zimshukie. Basi wakarudi na hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Ana ghadhabu juu yao kwa kumkanusha kwao Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, baada ya kuwa na ghadhabu juu yao kwa kuipotoa Taurati. Na wenye kukanusha unabii wa Muhammad, rehema na amani zimshukie, wana adhabu yenye kuwabadilisha na kuwafanya wanyonge
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek