Quran with Swahili translation - Surah Ta-Ha ayat 111 - طه - Page - Juz 16
﴿۞ وَعَنَتِ ٱلۡوُجُوهُ لِلۡحَيِّ ٱلۡقَيُّومِۖ وَقَدۡ خَابَ مَنۡ حَمَلَ ظُلۡمٗا ﴾
[طه: 111]
﴿وعنت الوجوه للحي القيوم وقد خاب من حمل ظلما﴾ [طه: 111]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na nyuso za viumbe zitamnyenyekea na kumdhalilikia mwenye kuziumba, Mwenye kila maana ya uhai mkamilifu kama inavyonasibiana na utukufu Wake, Ambaye Hafi , Anayesimama kuendesha kila kitu, Aliye Mkwasi wa kutomuhitajia asiyekuwa Yeye. Kwa kweli, amepata hasara Siku ya Kiyama mwenye kumfanya ni mshirika wa Mwenyezi Mungu yoyote kati ya viumbe Vyake |