Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 11 - الحج - Page - Juz 17
﴿وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَعۡبُدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ حَرۡفٖۖ فَإِنۡ أَصَابَهُۥ خَيۡرٌ ٱطۡمَأَنَّ بِهِۦۖ وَإِنۡ أَصَابَتۡهُ فِتۡنَةٌ ٱنقَلَبَ عَلَىٰ وَجۡهِهِۦ خَسِرَ ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةَۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡخُسۡرَانُ ٱلۡمُبِينُ ﴾
[الحج: 11]
﴿ومن الناس من يعبد الله على حرف فإن أصابه خير اطمأن به﴾ [الحج: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Miongoni mwa watu kuna anayeingia kwenye Uislamu kwa udhaifu na shaka, akawa anamuabudu Mwenyezi Mungu juu ya shaka na ukosefu wa uamuzi, ni kama yule anayesimama kwenye ukingo wa jabali au ukuta, hawi thabiti katika kusimama kwake, huifungamanisha Imani yake na ulimwengu wake: akiishi katika hali ya afya na ukunjufu huendelea kwenye ibada yake, na akipatikana na mitihani ya tabu na shida huyanasibisha hayo na Dini yake, na kwa hivyo huiacha. Ni kama yule anayegeuka kwa uso wake baada ya kulingana sawa, hivyo basi akapata hasara ya ulimwengu, kwani kukufuru kwake hakugeuzi chochote alichokadiriwa katika ulimwengu wake, na akapata hasara ya Akhera kwa kuingia Motoni, na hiyo ni hasara inayoonekana waziwazi |