Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 25 - الحج - Page - Juz 17
﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ ٱلَّذِي جَعَلۡنَٰهُ لِلنَّاسِ سَوَآءً ٱلۡعَٰكِفُ فِيهِ وَٱلۡبَادِۚ وَمَن يُرِدۡ فِيهِ بِإِلۡحَادِۭ بِظُلۡمٖ نُّذِقۡهُ مِنۡ عَذَابٍ أَلِيمٖ ﴾
[الحج: 25]
﴿إن الذين كفروا ويصدون عن سبيل الله والمسجد الحرام الذي جعلناه للناس﴾ [الحج: 25]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu na wakayakanusha yale ambayo alikuja nayo Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wakawazuia wengine kuingia kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu, wakamzuia Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, pamoja na waumini katika mwaka wa Ḥudaybiyah wasiingie Msikiti wa Ḥarām tulioufanya ni wa Waumini wote, wanaokaa hapo na wanaokuja kuukusudia, hao watapata adhabu kali yenye kuumiza. Na yoyote anayetaka, ndani ya Msikiti wa Ḥarām, kuenda kombo na haki kwa njia ya udhalimu na akamuasi Mwenezi Mungu humo ndani, basi tutamuonjesha adhabu kali yenye kuumiza |