×

Kwa kumtakasikia Imani Mwenyezi Mungu, bila ya kumshirikisha. Na anaye mshirikisha Mwenyezi 22:31 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-hajj ⮕ (22:31) ayat 31 in Swahili

22:31 Surah Al-hajj ayat 31 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 31 - الحج - Page - Juz 17

﴿حُنَفَآءَ لِلَّهِ غَيۡرَ مُشۡرِكِينَ بِهِۦۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَتَخۡطَفُهُ ٱلطَّيۡرُ أَوۡ تَهۡوِي بِهِ ٱلرِّيحُ فِي مَكَانٖ سَحِيقٖ ﴾
[الحج: 31]

Kwa kumtakasikia Imani Mwenyezi Mungu, bila ya kumshirikisha. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu ni kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, kisha ndege wakamnyakua au upepo ukamtupa pahala mbali

❮ Previous Next ❯

ترجمة: حنفاء لله غير مشركين به ومن يشرك بالله فكأنما خر من السماء, باللغة السواحيلية

﴿حنفاء لله غير مشركين به ومن يشرك بالله فكأنما خر من السماء﴾ [الحج: 31]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hali ya kulingana sawa kwa Mwenyezi Mungu juu ya kumtakasia matendo, kumuelekea Yeye kwa kumuabudu Yeye Peke Yake na kumpwekesha kwa utiifu na kumuepuka kila asiyekuwa Yeye kwa kukataa ushirikina, kwani mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu chochote, mfano wake- katika kuwa mbali kwake na uongofu na katika kuangamia kwake na kuanguka kwake kutoka kwenye kilele cha Imani hadi kwenye shimo la ukafiri na wakawa Mashetani wanamnyakuwa kutoka kila upande - ni kama mfano wa mtu aliyeanguka kutoka mbinguni, ima ndege watamnyakuwa na kumkatakata viungo vyake au kimbunga kikali cha upepo kitamchukua kimtupe mahali mbali sana
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek