Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 32 - الحج - Page - Juz 17
﴿ذَٰلِكَۖ وَمَن يُعَظِّمۡ شَعَٰٓئِرَ ٱللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقۡوَى ٱلۡقُلُوبِ ﴾
[الحج: 32]
﴿ذلك ومن يعظم شعائر الله فإنها من تقوى القلوب﴾ [الحج: 32]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hayo ndiyo Aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu ya kumpwekesha na kumtakasia ibada. Na yoyote mwenye kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na akayatukuza mambo makubwa ya Dini, na miongoni mwayo ni matendo ya Hija na sehemu zake na wanyama wanaochinjwa huko, kwa kuchagua walio wazuri na walio wanono, basi kutukuza huko ni katika vitendo vya wenye nyoyo zenye kusifika kwa kumcha Mwenyezi Mungu na kumuogopa |