Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 30 - الحج - Page - Juz 17
﴿ذَٰلِكَۖ وَمَن يُعَظِّمۡ حُرُمَٰتِ ٱللَّهِ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّهُۥ عِندَ رَبِّهِۦۗ وَأُحِلَّتۡ لَكُمُ ٱلۡأَنۡعَٰمُ إِلَّا مَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡۖ فَٱجۡتَنِبُواْ ٱلرِّجۡسَ مِنَ ٱلۡأَوۡثَٰنِ وَٱجۡتَنِبُواْ قَوۡلَ ٱلزُّورِ ﴾
[الحج: 30]
﴿ذلك ومن يعظم حرمات الله فهو خير له عند ربه وأحلت لكم﴾ [الحج: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hiyo Aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu ya kuondoa uchafu, kutekeleza nadhiri na kuitufu Nyumba ndiyo Aliyoyapasisha Mwenyezi Mungu, basi yatukuzeni. Na yoyote mwenye kuyatukuza Aliyoyatakasa Mwenyezi Mungu, na miongoni mwayo ni matendo Aliyoyawekea ibada ya Hija kwa kuyatekeleza kikamilifu kwa kumtakasia Mwenyezi Mungu, basi hilo ni bora zaidi kwake, ulimwenguni na Akhera. Na Mwenyezi Mungu Amewahalalishia nyinyi kula wanyama-howa isipokuwa kile Alichokiharamisha kwenu katika kile mnachosomewa ndani ya Qur’ani miongoni mwa mizoga na mengineyo, basi kiepukeni. Katika hili pana kubatilisha kile ambacho Waarabu walikuwa wakikiharamisha cha baadhi ya wanyama-howa. Na jiekeni mbali na uchafu ambao ni masanamu na urongo wa kumzulia Mwenyezi Mungu |