×

Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa ni kudhihirisha matukuzo kwa Mwenyezi Mungu; 22:36 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-hajj ⮕ (22:36) ayat 36 in Swahili

22:36 Surah Al-hajj ayat 36 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 36 - الحج - Page - Juz 17

﴿وَٱلۡبُدۡنَ جَعَلۡنَٰهَا لَكُم مِّن شَعَٰٓئِرِ ٱللَّهِ لَكُمۡ فِيهَا خَيۡرٞۖ فَٱذۡكُرُواْ ٱسۡمَ ٱللَّهِ عَلَيۡهَا صَوَآفَّۖ فَإِذَا وَجَبَتۡ جُنُوبُهَا فَكُلُواْ مِنۡهَا وَأَطۡعِمُواْ ٱلۡقَانِعَ وَٱلۡمُعۡتَرَّۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرۡنَٰهَا لَكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ ﴾
[الحج: 36]

Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa ni kudhihirisha matukuzo kwa Mwenyezi Mungu; kwa hao mna kheri nyingi. Basi litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao wanapo simama kwa safu. Na waangukapo ubavu kuleni katika hao na walisheni walio kinai na wanao lazimika kuomba. Ndio kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru

❮ Previous Next ❯

ترجمة: والبدن جعلناها لكم من شعائر الله لكم فيها خير فاذكروا اسم الله, باللغة السواحيلية

﴿والبدن جعلناها لكم من شعائر الله لكم فيها خير فاذكروا اسم الله﴾ [الحج: 36]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na tumewafanyia nyinyi kule kuchinja ngamia ni miongoni mwa alama za Dini na mambo yake makubwa. Ili mpate kujisongeza karibu na Mwenyezi Mungu kwayo. Katika hao nyinyi, enyi wenye kujisongeza karibu naye, muna kheri katika manufaa yake ya kula, kutoa sadaka na kupata malipo ya thawabu. Basi semeni mnapowachinja, «Bismillāh» (kwa jina la Mwenyezi Mungu). Na ngamia huchinjwa akiwa amesimama, miguu yake mitatu imepangwa na mmoja umefungwa, basi akianguka kwa mbavu zake, huwa amekuwa halali kumla. Wale waliomchinja kwa ajili ya ibada na wale kitu katika mnyama huyo na wamlishe kutokana naye aliyekinai, naye ni muhitaji asiyeomba kwa kujihifadhi, na muhitaji anayeomba kumaliza haja yake. Hivi ndivyo Alivyowadhalilishia Mwenyezi Mungu ngamia, huenda mukamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwadhalilishia
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek