×

Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia uchamngu wenu. 22:37 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-hajj ⮕ (22:37) ayat 37 in Swahili

22:37 Surah Al-hajj ayat 37 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 37 - الحج - Page - Juz 17

﴿لَن يَنَالَ ٱللَّهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَآؤُهَا وَلَٰكِن يَنَالُهُ ٱلتَّقۡوَىٰ مِنكُمۡۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمۡ لِتُكَبِّرُواْ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمۡۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ﴾
[الحج: 37]

Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia uchamngu wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyo kuongoeni. Na wabashirie wafanyao mema

❮ Previous Next ❯

ترجمة: لن ينال الله لحومها ولا دماؤها ولكن يناله التقوى منكم كذلك سخرها, باللغة السواحيلية

﴿لن ينال الله لحومها ولا دماؤها ولكن يناله التقوى منكم كذلك سخرها﴾ [الحج: 37]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hazitamfikia Mwenyezi Mungu nyama za vichinjwa hivyi wala damu zake kitu chochote, kitakachomfikia Yeye ni kule kumtakasia kwenu katika hivyo na kuwa lengo lake ni radhi za Mwenyezi Mungu Peke Yake. Hivyo basi Amewadhalilishia nyinyi, enyi wenye kujikurubisha, ili mumtukuze Mwenyezi Mungu na mumshukuru kwa kuwaongoza kwenye haki, kwani Yeye Anastahiki hilo. Na uwape bishara njema, ewe Nabii, wenye kufanya wema kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake na kuwafanyia wema viumbe vyake, kupata kila lema na kufaulu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek