Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 47 - الحج - Page - Juz 17
﴿وَيَسۡتَعۡجِلُونَكَ بِٱلۡعَذَابِ وَلَن يُخۡلِفَ ٱللَّهُ وَعۡدَهُۥۚ وَإِنَّ يَوۡمًا عِندَ رَبِّكَ كَأَلۡفِ سَنَةٖ مِّمَّا تَعُدُّونَ ﴾
[الحج: 47]
﴿ويستعجلونك بالعذاب ولن يخلف الله وعده وإن يوما عند ربك كألف سنة﴾ [الحج: 47]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na makafiri wa Kikureshi, kwaujinga wao, wanakuharakisha, ewe Mtme, uwaletee adhabu ambayo uliwaonya nayo baada ya kuwa wakakamavu juu ya ukafiri. Mwenyezi Mungu Hataenda kinyume na ahadi yake ya adhabu aliyowaonya nayo, haina budi kutuka. Na hapa duniani Aliwaharakishia hiyo, siku ya vita vya Badr. Na siku moja miongoni mwa siku mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama miaka alfu moja mnazozihesbu katika miaka duniani |