Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 65 - الحج - Page - Juz 17
﴿أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَٱلۡفُلۡكَ تَجۡرِي فِي ٱلۡبَحۡرِ بِأَمۡرِهِۦ وَيُمۡسِكُ ٱلسَّمَآءَ أَن تَقَعَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِٱلنَّاسِ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ ﴾
[الحج: 65]
﴿ألم تر أن الله سخر لكم ما في الأرض والفلك تجري في﴾ [الحج: 65]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amewadhalilishia vilivyoko ardhini miongoni mwa vitu vitambaavyo na wanyama na nafaka na matunda na vitu visivyo na roho, kwa ajili ya kipando chenu, chakula chenu na manufaa yenu, kama Alivyowadhalilishia mashua zinazotembea baharini kwa uweza Wake na amri Yake, ziwabebe nyinyi na vyombo vyenu ziwafikishe kwenye miji na sehemu mzitakazo na kwamba Yeye Ndiye Anayeizuia mbingu na kuitunza, ili isianguke juu ya ardhi ikawaangamiza walioko juu yake isipokuwa kwa idhini Yake, Aliyetakasika na kila sifa za upungufu, kuwa hilo lifanyike, ili Awarehemu watu rehema kunjufu katika mambo yao ya hivi sasa hapa duniani na ya baadaye kesho Akhera? Na miongoni mwa rehema Zake ni vitu hivi Alivowadhalilishia na vinginevyo kwa fadhila Zake juu yao |