Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 64 - الحج - Page - Juz 17
﴿لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ ﴾
[الحج: 64]
﴿له ما في السموات وما في الأرض وإن الله لهو الغني الحميد﴾ [الحج: 64]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ni vya Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, vilivyoko ardhini na mbinguni, kwa kuviumba, kuvimiliki na kuwa chini ya usimamizi wake, kila kimoja kati ya hizo kinahitajia uendeshaji Wake na maneemesho Yake. Na hakika Mwenyezi Mungu Ndie Aliye Mkwasi ambaye Hahitajii kitu chochote, Anayeshukuriwa kwa kila namna |