Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 71 - الحج - Page - Juz 17
﴿وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗا وَمَا لَيۡسَ لَهُم بِهِۦ عِلۡمٞۗ وَمَا لِلظَّٰلِمِينَ مِن نَّصِيرٖ ﴾
[الحج: 71]
﴿ويعبدون من دون الله ما لم ينـزل به سلطانا وما ليس لهم﴾ [الحج: 71]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na makafiri wa Kikureshi wanashikilia kumshirikisha Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa ubatilifu wa waliyonayo uko waziwazi. Wao wanawaabudu waungu ambao haukuteremka, kwenye kitabu chochote miongoni mwa vitabu vya Mwenyezi Mungu, ushahidi kuwa wao wanafaa kufanyiwa ibada, na wao (hao waungu) hawajui chochote kuhusu yale waliyoyazua (hao makafiri) na kumsingizia Mwenyezi Mungu, hakika hilo ni jambo ambalo kwalo wamewafuata baba zao bila dalili yoyote. Basi kitakapokuja kipindi cha kuhesabiwa huko Akhera, hawa washirikina hawatakuwa na msaidizi mwenye kuwanusuru au kuwakinga na adhabu |