Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 72 - الحج - Page - Juz 17
﴿وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُنَا بَيِّنَٰتٖ تَعۡرِفُ فِي وُجُوهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلۡمُنكَرَۖ يَكَادُونَ يَسۡطُونَ بِٱلَّذِينَ يَتۡلُونَ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِنَاۗ قُلۡ أَفَأُنَبِّئُكُم بِشَرّٖ مِّن ذَٰلِكُمُۚ ٱلنَّارُ وَعَدَهَا ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ ﴾
[الحج: 72]
﴿وإذا تتلى عليهم آياتنا بينات تعرف في وجوه الذين كفروا المنكر يكادون﴾ [الحج: 72]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na pindi zinaposomwa kwa washirikina aya za Qur’ani zilizo wazi, utauona uchukivu waziwazi kwenye nyuso zao, wanakaribia kuwapiga Waumini wanaowalingania kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kuwasomea aya Zake. Basi waambie, ewe Mtume, «je, si niwape habari ya kitu chenye kuchukiza zaidi kwenu kuliko kuisikia haki na kuwaona walinganizi wake? Ni Moto ambao Mwenyezi Mungu Ameutayarisha kwa makafiri huko Akhera. Na mahali pabaya zaidi pa mtu kuishia ni hapo.» |