Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 15 - النور - Page - Juz 18
﴿إِذۡ تَلَقَّوۡنَهُۥ بِأَلۡسِنَتِكُمۡ وَتَقُولُونَ بِأَفۡوَاهِكُم مَّا لَيۡسَ لَكُم بِهِۦ عِلۡمٞ وَتَحۡسَبُونَهُۥ هَيِّنٗا وَهُوَ عِندَ ٱللَّهِ عَظِيمٞ ﴾
[النور: 15]
﴿إذ تلقونه بألسنتكم وتقولون بأفواهكم ما ليس لكم به علم وتحسبونه هينا﴾ [النور: 15]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kipindi mlichokuwa mnaupokea uzushi na mnaueneza kwa midomo yenu, nao ni yale maneno ya urongo na ambayo hamuna ujuzi nao. Na mambo mawili haya yameharamishwa: kusema maneno ya urongo na kusema bila ya ujuzi. Na mnadhani kuwa hilo ni jambo dogo, nalo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Katika haya pana makemeo bayana juu ya kupuuza makatazo ya uenezaji ubatilifu |