Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 28 - النور - Page - Juz 18
﴿فَإِن لَّمۡ تَجِدُواْ فِيهَآ أَحَدٗا فَلَا تَدۡخُلُوهَا حَتَّىٰ يُؤۡذَنَ لَكُمۡۖ وَإِن قِيلَ لَكُمُ ٱرۡجِعُواْ فَٱرۡجِعُواْۖ هُوَ أَزۡكَىٰ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِيمٞ ﴾
[النور: 28]
﴿فإن لم تجدوا فيها أحدا فلا تدخلوها حتى يؤذن لكم وإن قيل﴾ [النور: 28]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na iwapo hamtampata mtu kwenye nyumba za watu wengine, basi msizingie mpaka aweko mwenye kuwaruhusu. Asiporuhusu na akasema, «rudini,» basi rudini, wala msisisitize kutaka kuruhusiwa, kwani kurudi wakati huo ni jambo zuri zaidi kwenu, kwani mwanadamu ana nyakati na hali ambazo hapendi kwenye hali hizo kuonekana na mtu mwingine. Na Mwenyezi Mungu kwa mnayoyatenda ni Mjuzi na Atamlipa kila mtendaji kitendo chake |