Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 3 - النور - Page - Juz 18
﴿ٱلزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوۡ مُشۡرِكَةٗ وَٱلزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَآ إِلَّا زَانٍ أَوۡ مُشۡرِكٞۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ﴾
[النور: 3]
﴿الزاني لا ينكح إلا زانية أو مشركة والزانية لا ينكحها إلا زان﴾ [النور: 3]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwanamume mzinifu haridhiki isipokuwa kumuoa mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina asiyekubali uharamu wa uhalifu wa uzinifu, na mwanamke mzinifu haridhiki isipokuwa kuolewa na mwanamume mzinifu mwanamume mshirikina asiyekubali uharamu wa uzinifu. Ama wanaume na wanawake wanaojizuia na uzinifu, wao hawaridhiki na hilo, na ndoa hiyo imeharamishwa kwa Waumini. Na huu ni ushahidi wazi wa uharamu wa kumuoa mwanamke mzinifu mpaka atubie, vilevile uharamu wa kumuoza mwanamume mzinifu mpaka atubie |