×

Na walio kufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu 24:39 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nur ⮕ (24:39) ayat 39 in Swahili

24:39 Surah An-Nur ayat 39 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 39 - النور - Page - Juz 18

﴿وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَعۡمَٰلُهُمۡ كَسَرَابِۭ بِقِيعَةٖ يَحۡسَبُهُ ٱلظَّمۡـَٔانُ مَآءً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَهُۥ لَمۡ يَجِدۡهُ شَيۡـٔٗا وَوَجَدَ ٱللَّهَ عِندَهُۥ فَوَفَّىٰهُ حِسَابَهُۥۗ وَٱللَّهُ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ ﴾
[النور: 39]

Na walio kufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote. Na atamkuta Mwenyezi Mungu hapo naye amlipe hisabu yake sawa sawa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: والذين كفروا أعمالهم كسراب بقيعة يحسبه الظمآن ماء حتى إذا جاءه لم, باللغة السواحيلية

﴿والذين كفروا أعمالهم كسراب بقيعة يحسبه الظمآن ماء حتى إذا جاءه لم﴾ [النور: 39]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na wale waliomkanusha Mola wao na wakawafanya warongo Mitume Wake, matendo yao waliyoyategemea kuwa yatawafaa huko Akhera, kama kuunga kizazi, kuwaacha huru mateka na yasiyokuwa hayo, yatakuwa ni kama mangati, nayo ni yale yanayoonekana kama maji juu ya ardhi tambarare kipindi cha mchana cha jua kali, mwenye kiu akiyaona anadhani ni maji, na akiyajia hakuti kuwa ni maji. Basi kafiri anadhani kwamba matendo yake yatamfaa, na ifikapo Siku ya Kiyama atakuta kuwa hayana malipo mema, na hapo atamkuta Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Anamngojea Ampe malipo ya matendo yake kikamilifu. Na Mwenyezi Mungu ni Mpesi wa kuhesabu. Basi wajinga wasione kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu imekawia kuwa, kwani hiyo hapana budi kuja kwake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek