Quran with Swahili translation - Surah Al-Furqan ayat 31 - الفُرقَان - Page - Juz 19
﴿وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوّٗا مِّنَ ٱلۡمُجۡرِمِينَۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيٗا وَنَصِيرٗا ﴾
[الفُرقَان: 31]
﴿وكذلك جعلنا لكل نبي عدوا من المجرمين وكفى بربك هاديا ونصيرا﴾ [الفُرقَان: 31]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kama tulivyokufanya, ewe Mtume, uwe na maadui miongoni mwa wahalifu watu wako, tulimfanya kila Nabii, miongoni mwa Manabii, awe na adui kati ya wale wahalifu wa watu wake. Basi vumilia kama walivyovumilia. Na inatosha kuwa Mola wako ni Mwenye kuongoa, ni Mwenye kuilekeza, ni Mwenye kuonyesha njia na ni Mwenye kutoa msaada wa kukusaidia wewe dhidi ya maadui zako.Katika haya pana maliwazo kwa Nabii Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye |