Quran with Swahili translation - Surah Al-Furqan ayat 30 - الفُرقَان - Page - Juz 19
﴿وَقَالَ ٱلرَّسُولُ يَٰرَبِّ إِنَّ قَوۡمِي ٱتَّخَذُواْ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ مَهۡجُورٗا ﴾
[الفُرقَان: 30]
﴿وقال الرسول يارب إن قومي اتخذوا هذا القرآن مهجورا﴾ [الفُرقَان: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mtume atasema akishtakia matendo ya watu wake, «Ewe Mola wangu! Kwa kweli watu wangu wameiacha hii Qur’ani na wameigura, wameendelea sana katika kuipa mgongo na kuacha kuizingatia na kuitumia na kuifikisha. Katika aya hii pana kitisho kikubwa kwa anayeigura Qur’ani na asiitumie |