Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 52 - النَّمل - Page - Juz 19
﴿فَتِلۡكَ بُيُوتُهُمۡ خَاوِيَةَۢ بِمَا ظَلَمُوٓاْۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ ﴾
[النَّمل: 52]
﴿فتلك بيوتهم خاوية بما ظلموا إن في ذلك لآية لقوم يعلمون﴾ [النَّمل: 52]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hayo ni makazi yao, yako matupu, hakuna yoyote ndani yake. Mwenyezi Mungu Amewaangamiza kwa sababu ya wao kuzidhulumu nafsi zao kwa ushirikina na kumkanusha Nabii wao. Kwa kweli, katika uvunjaji huo na uangamizaji pana mawaidha kwa watu wanaokijua kile tulichowafanya. Na huu ndio mwendo wetu kwa wenye kuwakanusha Mitume |