Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 8 - النَّمل - Page - Juz 19
﴿فَلَمَّا جَآءَهَا نُودِيَ أَنۢ بُورِكَ مَن فِي ٱلنَّارِ وَمَنۡ حَوۡلَهَا وَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴾
[النَّمل: 8]
﴿فلما جاءها نودي أن بورك من في النار ومن حولها وسبحان الله﴾ [النَّمل: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mūsā alipoujia moto, Mola wake Alimwita na akampa habari kwamba hapa ni mahali Alipopatakasa Mwenyezi Mungu na Akapabariki na Akapafanya ni mahali pa kusema na Mūsā na kumtumiliza, na kwamba Mwenyezi Mungu Amewabariki waliopo motoni na waliopo pambizoni mwake miongoni mwa Malaika, na kumtakasa Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe, kwa kumuepusha na sifa zisizonasibiana na Yeye |