Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 92 - النَّمل - Page - Juz 20
﴿وَأَنۡ أَتۡلُوَاْ ٱلۡقُرۡءَانَۖ فَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهۡتَدِي لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَقُلۡ إِنَّمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُنذِرِينَ ﴾
[النَّمل: 92]
﴿وأن أتلو القرآن فمن اهتدى فإنما يهتدي لنفسه ومن ضل فقل إنما﴾ [النَّمل: 92]
Abdullah Muhammad Abu Bakr na niwasomee watu Qur’ani, basi mwenye kuongoka kuyajua yaliyomo ndani yake na akayafuata niliokuja nayo, wema wa hilo na malipo yake yatamfaa mwenyewe. Na mwenye kupotea akapotoka na njia ya haki, basi wewe sema, «Mimi ni muonyaji kwenu, nawaonya na adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso Yake iwapo hamtaamini, kwani mimi ni mmoja wa Mitume waliowaonya watu wao, na uongofu wa aina yoyote hauko mikononi mwangu |