Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 91 - النَّمل - Page - Juz 20
﴿إِنَّمَآ أُمِرۡتُ أَنۡ أَعۡبُدَ رَبَّ هَٰذِهِ ٱلۡبَلۡدَةِ ٱلَّذِي حَرَّمَهَا وَلَهُۥ كُلُّ شَيۡءٖۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ ﴾
[النَّمل: 91]
﴿إنما أمرت أن أعبد رب هذه البلدة الذي حرمها وله كل شيء﴾ [النَّمل: 91]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu, «Hakika nimeamrishwa nimuabudu Mola wa mji huu, nao ni Makkah, ambao Ameuharamisha kwa viumbe wake wasimwage humo damu iliyo haramu kuimwaga au kumdhulumu yoyote ndani yake au kuwinda viindwa vyake au kukata mti wake. Na ni Chake Yeye kila kitu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake. Na nimeamrishwa nimuabudu Yeye Peke Yake, na sio mwingine, na niwe mtiifu Kwake |