Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 43 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ مِنۢ بَعۡدِ مَآ أَهۡلَكۡنَا ٱلۡقُرُونَ ٱلۡأُولَىٰ بَصَآئِرَ لِلنَّاسِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لَّعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ ﴾
[القَصَص: 43]
﴿ولقد آتينا موسى الكتاب من بعد ما أهلكنا القرون الأولى بصائر للناس﴾ [القَصَص: 43]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hakika tulimpa Mūsā Taurati baada ya kuwaangamiza ummah waliokuwa kabla yake, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād, Thamūd, na watu wa Lūṭ na watu wa Madyan, hali ya kuwa Taurati ina hoja kwa Wana wa Isrāīl ambazo kwa hizo wanayaona yale yanayowafaa na yanayowadhuru, na ndani yake kuna rehema kwa wanaoifuata Taurati kivitendo. Huenda wao wakazikumbuka neema za Mweyezi Mungu juu yao, wakamshukuru kwa hizo na wasimkanushe |