Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 54 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿أُوْلَٰٓئِكَ يُؤۡتَوۡنَ أَجۡرَهُم مَّرَّتَيۡنِ بِمَا صَبَرُواْ وَيَدۡرَءُونَ بِٱلۡحَسَنَةِ ٱلسَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ ﴾
[القَصَص: 54]
﴿أولئك يؤتون أجرهم مرتين بما صبروا ويدرءون بالحسنة السيئة ومما رزقناهم ينفقون﴾ [القَصَص: 54]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hawa ambao sifa zao zimetangulia, watapewa malipo ya matendo yao mema mara mbili: ya kukiamini Kitabu chao na kuiamini kwao Qur’ani kwa vile walivyosubiri. Na miongoni mwa sifa zao ni kwamba wao wanalikinga baya kwa zuri, na katika kile tunachowaruzuku wanatumia katika njia ya uzuri na wema |