Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 55 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿وَإِذَا سَمِعُواْ ٱللَّغۡوَ أَعۡرَضُواْ عَنۡهُ وَقَالُواْ لَنَآ أَعۡمَٰلُنَا وَلَكُمۡ أَعۡمَٰلُكُمۡ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡ لَا نَبۡتَغِي ٱلۡجَٰهِلِينَ ﴾
[القَصَص: 55]
﴿وإذا سمعوا اللغو أعرضوا عنه وقالوا لنا أعمالنا ولكم أعمالكم سلام عليكم﴾ [القَصَص: 55]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanaposikia, watu hawa, maneno ya ubatilifu, hawayapulikizi, na wanasema, «Sisi tuna matendo yetu tusiyoyaepuka, na nyinyi muna matendo yenu msiyoyaepuka. Sisi hatujishughulishi kuwarudi nyinyi, na hamtasikia kutoka kwetu isipokuwa mema, na hatutasema na nyinyi kulingana na ujinga wenu, kwa kuwa sisi hatutaki njia ya wajinga na hatuipendi.» Na haya ni miongoni mwa maneno mazuri zaidi ambayo walinganizi kwa Mwenyezi Mungu wanayasema |